MAMBO YAKUANGALIA KATIKA UWEKEZAJI WA NYUMBA
Karibu katika blog hii ya maswala ya nyumba kitu ambacho watu wengi wanajua ni kuwa kuna utajiri mkubwa sana katika makazi. Kwa maana kihistoria ni kwamba mpaka sas utajiri wa karibia asilimia 70% umepatikana kwenye Real Estate yaani nyumba na shughuli zinzoendana na hivyo. Sehumu nyingi duniani kutokana na umuhimu wake sector hii iko rasmi sana ingawa kwa hapa kwetu imekuwa hajachukua mfumo huo ila kwa sasa mambo yanabadilika kwa kiasi kikubwa ni moja ya malengo ya page hii iwe inafuatilia hayo mabadiliko ya kuyaleta hapa watu wayajadili na kuwa na taratibu nzuri za kufanya mambo. Na jambo lingine kutokana na sheria ya mortgage kuanza kufanya kazi vile vile mabenki kadhaa nayo yameanza kukopesha mikopo ya muda mrefu. Ni vyema kujua taratibu na jinsi ya kujiweka kuweza kufanikisha kupata mikopo hiyo. Hii ni sector pekee duniani ambao watu wako tayari kukupa fedha kwa kuweka hiyo hiyo dhamana unayokopea kwa hiyo ikijipanga vizuri utakuwa katika nafasi njema ...